Ijumaa , 7th Aug , 2015

Kiungo wa Yanga, Hassan Dilunga amesaini mkataba wa mwaka mmoja wa kuitumikia Ruvu Shooting katika msimu mpya wa Ligi Daraja la kwanza Tanzania Bara.

Dilunga hakuwa na namba ya kudumu katika kikosi cha Yanga msimu uliopita kutokana na kukabiliwa na ushindani mkubwa kutoka kwa viungo wengine mahiri wa timu hiyo.

Kiungo huyo alivunja mkataba na Yanga baada ya kutokea hali ya kutoelewana na uongozi wa timu hiyo kuhusiana na mustakabali wake ambapo timu hiyo ilipanga kumtoa kwa mkopo Dilunga katika kikosi cha Stand United kitendo kilichopingwa na mchezaji huyo ambaye litaka atemwe jumla.