Alhamisi , 9th Sep , 2021

Novak Djokovic ataendelea kuwania Grand Slam ya nne mwaka huu atakapovaana na bingwa wa Olimpiki Alexander Zverev mchezo wa nusu fainali ya US Open utakaopigwa siku ya Ijumaa.

Novak Djokovic akishangilia ushindi

Kinara huyo kwenye viwango vya ubora Duniani amefuzu nusu fainali baada ya kumnyuka Matteo Berrettini kwa seti 5-7, 6-2,6-2,6-3 .

Zverev ambaye anashikilia nafasi ya nne kwenye viwango vya ubora Duniani ndiye aliyeizima ndoto ya Djokovic katika michuano ya Olimpiki baada ya kumtupa nje katika nusu fainali.

Iwapo Djokovic atashinda US Open atakamilisha kibindoni Grand Slam nne baada ya kufanikiwa kutwaa Australian Open, French Open na Wimbledon mapema mwaka huu.