Jumanne , 27th Apr , 2021

Nyota wa timu ya kikapu ya Dallas Mavericks, Luka Doncic na Bradley Beal wa Washington Wizard wamechaguliwa kuwa wachezaji nyota wa wiki ya 18 katika ligi ya kikapu nchini Mreakani baaada ya wawili hao kuonesh aviwango bora katika wiki iliyoanzia Aprili 21 hadi Aprili 25, 2021.

Luka Doncic wa Dallas Mavericks (kushoto) na Bradley Beal wa Washington Wizard (Kulia).

Doncic ameibuka nyota kwa upande wa Magharibi baada na wastani wa kupata alama 26.0, rebaundi 10.0 na assisti 9.0  na kuisaidiaa timu yake kushinda michezo mitatu mfululizo na kushika nafasi ya 6 kwenye msimamo wa NBA kwa Upande wa Magharibi.

Kwa upande wa Mashabriki, Bradley Beal ameibuka kidedea baada ya kufikisha wastani wa alama 31.3, rebaundi 5.8 na kuisaidia timu yake kushinda michezo minne mfululizo kwenye juma hilo na kushika nafasi ya 10 ambapo bado wapo kwenye nafasi ya kucheza michezo ya mtoano.

NBA itaendelea tena usiku wa kuamkia kesho kwa michezo 6, Boston Celtics itacheza na Oklahoma City Thunder saa 8:00 usiku, Toronto Raptors itakipiga na Brooklyn Nets saa 8:30 usiku wakati ambao Golden State Warriors wataumana na Dallas Mavericks saa 10:30 Alfajiri.