Error message

  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 664 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 675 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 679 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).

Dr. Tiboroa kumrudisha Manji kivingine Yanga

Alhamisi , 10th Jan , 2019

Mgombea wa nafasi ya Uenyekiti wa klabu ya Yanga, Dr. Jonas Tiboroa amejinasibu kurejesha mfumo wa zamani wa klabu hiyo ambao utaruhusu klabu kuwa na kampuni mbili za kibiashara.

Dr. Jonas Tiboroa na Yusuph Manji

Katika muendelzo wa kampeni zake kuelekea uchaguzi huo, Dr. Tiboroa amesisitiza kuwa klabu ya Yanga itaendelea kuwa ya wanachama huku kukiwa na kampuni mbili, kampuni moja itakuwa inahusika katika uwekezaji na nyingine ambayo itahusika na biashara za klabu.

"Mimi nilipokuwa Katibu Mkuu chini ya Manji tulisema tutahakikisha kuwa Yanga inakuwa klabu ya wanachama na tukaanzisha kampuni mbili, moja inayoshughulikia uwekezaji na nyingine inayoshughulikia biashara za klabu", amesema.

"Hizi kampunni tulizisajili mwaka 2015, lakini kwa bahati mbaya kizo kampuni zote hazijafanya kazi mpaka sasa, ndiyo maana mimi nimeona kuna haja ya kurudi nikaendeleze yale niliyoyaanza", ameongeza Dr. Tiboroa.

Endapo Dr. Tiboroa atachaguliwa na mpango huo kukamilika, maana yake wawekezaji kama Yusuph Manji na wengine wanaweza kupata nafasi ya nafasi ya kuwekeza katika klabu hiyo bila kuathiri mfumo wake wa uanachama kwakuwa shughuli zote zitaratibiwa chini ya kampuni ya uwekezaji ya klabu.

Uchaguzi wa Yanga unatarajia kufanyika Januari 13, 2019 kwenye ukumbi wa bwalo la maafisa wa polisi Oysterbay Dar es salaa, ambapo nafasi ya Uenyekiti wa klabu inashindaniwa na wagombea  wawili, Dr. Jonas Tiboroa na Baraka Igangula. 

HABARI ZAIDI

Mabaki ya gari aina ya Noah iliyopata ajali Morogoro

Ajali yachukua uhai wa watu saba Morogoro

Waziri wa Fedha Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba

Wawekezaji wawekeze sekta za uzalishaji - Nchemba

Muonekano wa Kiburugwa ambako Nyumba zaidi ya Tisa Zimebomolewa na Maporomoko ya Tope

Maporomoko ya udongo yasomba nyumba 9 Mbagala

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko

Serikali yaipongeza Red Cross

Waziri wa TAMISEMI Mohamed Mchengerwa

Aonya wanaochangia watumishi kutopanda madaraja

Edgar Lungu, Rais wa Zamani Nchini Zambia Akitembea Kuzunguka Mji Mkuu wa Lusaka

Rais wa zamani Zambia Bw. Lungu hatarini kukamatwa

Mkuu wa Ulinzi Ukraine (Picha ya Website)

Zelensky amfukuza kazi mkuu wake wa ulinzi

Baadhi ya Wananchi wa Chindi na Ntinga wakiwa katika Harakati za Kuvuka Mto

Walazimika kulipa hadi 8000 kuvuka mto kwa mtumbwi