Jumatano , 20th Jun , 2018

Kuelekea kuanza kwa mashindano ya mpira wa Kikapu ya Sprite Bball Kings yanayoandaliwa na East Africa Television Limited, chini ya udhamini wa Kampuni ya Cocacola, kupitia kinywaji cha Sprite leo Juni 20, imefanyika droo ya hatua ya mtoano.

Waamuzi kutoka TBF Gozbert Boniface na Prosper Mushi wakiendesha droo ya mechi za mtoano.

Katika droo hiyo jumla ya timu 50 zimepangwa kuchuana ili kuwatafuta washindi 15, ambao wataungana na bingwa mtetezi kwaajili ya hatua ya 16 bora ya mashindano hayo ambayo yanafanyika kwa mara ya pili.

Droo hiyo iliyofanyika kwenye ofisi za East Africa Television, iliongozwa na Kamishna wa Ufundi na Mipango wa Shirikisho la Mpira wa Kikapu Tanzania (TBF), Manase Zablon pamoja na wawakilishi wa timu hizo 50. 

Wawakilishi wa timu shiriki wakifuatilia kwa umakini droo ya mechi ya mtoano.

Kabla ya droo kufanyika timu zote zilisomewa Sheria na kanuni za mashindano kwa msimu huu ambapo wote kwa pamoja walikubaliana na sheria hizo. Moja ya sheria hizo ni timu inaruhusiwa kuwachezesha kwa pamoja wachezaji wawili tu wa daraja la kwanza.

Mechi za hatua ya mtoano zitaanza kutimua vumbi kuanzia Juni 30, 2018. Mechi hizo ni kama zinavyoonekana hapo chini.

1. Dream Chaser   Vs TMK Heroes
2. The Fighter  Vs Force One
3. Flying Dribblers Vs Kurasini Worriors
4. TMT Vs Street Ballers
5. GWU  Vs External Heroes
6. DMI Vs Madale State
7. Ardhi University Vs The Kazi 8 Lycans
8. Ukonga Worriors Vs Little Saint
9. Oysterbay Vs  Ilala Easzone
10. BTP Vs Grounders
11. Oratory Vs Mbezi Beach KKKT
12. The Sniper Vs Young Boys
13. Eagle Wings Vs Portland
14. Golden Talent  Vs  Montefort Kings
15. Ukonga Hitmen Vs Yombo Patroit
16. The Hashtag Vs BV
17. Bankers Vs Water Insititute
18. NIT Ballers Vs Air Wings
19. Fast Heat Vs Street Worriors
20. Stylers Vs Denth Shoppers
21. Loyo Light Vs  Kigamboni City
22. K-Worriors  Vs  Team Kiza
23. Madena  Vs St. Joseph
24. The Magic Vs  Raptors
25. Weusi Vs Kichangani