Jumanne , 15th Feb , 2022

Seth Curry na Andre Drummond wamesaidia kuipa ushindi wa kwanza Brooklyn Nets wa alama 109 kwa 85 dhidi ya timu ngumu ya Sacramento Kings alfajiri ya kuamkia leo Jumanne Februari 15 baada ya vichapo 11 mfululizo kwenye NBA.

(Andre Drummond wakipongezana na Seth Curry baada ya kuifungia Nets)

Mchezo huo ni mchezo wa kwanza kwa wawili hao waliojiunga na Brooklyn Wiki iliyopita wakitokea Philadelphia 76ers na kuonesha kiwango kizuri ambapo Seth Curry amefunga alama 23, rebound 7 na Assist 5.

Andre Drummond amefunga alama 11, rebound 9 na Assist 4 alama ambazo zimeifanya Brooklyn kutoka kutoka nafasi ya 11 kupanda hadi nafasi ya nane ambapo wanawania kumaliza katika nafasi hizo ili wacheze NBA Playoffs.