Alhamisi , 16th Dec , 2021

Anthony Edwards ameweka rekodi ya kuwa mcheza kikapu mwenye umri mdogo zaidi kufunga alama tatu mara 10 kwenye mchezo mmoja katika historia ya NBA na kumpiku Kyrie Irving aliyefanya hivyo mwaka 2015 alipokuwa na miaka 22.

(Anthony Edwards akijaribu kumtoka Nikol Jokic wa Denver Nuggets)

Edwards mwenye miaka 20, ameweka rekodi hiyo alfajiri ya kuamkia leo wakati alipokuwa anaichezea timu yake ya Minnesota Timberwolves na kuisaidia kuibuka na ushindi wa alama 124-107 dhidi ya Denver Nuggets.

(Anthony Edwards akishangilia baada ya kufunga moja ya 3-point na kuipa timu yake ushindi)

Mbali na rekodi hiyo, Edwards pia ameweka rekodi ya kuwa mchezaji wanne kwenye historia ya NBA kufunga alama 2,000 kwa haraka zaidi kuliko mchezaji yeyote kwani ametumia michezo 72 tokea aanza kucheza msimu wa 2020-2021.