
Afisa Habari wa Shirikisho la Soka nchini TFF Alfred Lucas amesema, Mali imeondolewa katika fainali hizo kutokana na migogoro ndani ya uongozi wa Chama Cha Soka nchini humo uliofanya Serikali iingilie kati na sasa katika kundi hilo kuna timu za "Serengeti Boys", Algeria, Ethiopia na Angola," amesema Alfredy Lucas.
Alfred amesema kuwa, kuelekea katika mashindano hayo, kikosi cha Serengeti Boys kinaendelea na mazoezi kwaajili ya maandalizi ya michezo miwili ya kimataifa ya kirafiki dhidi ya Gabon na baadaye Morocco na Cameroon.
"Maandalizi yapo vizuri na vijana wapo vizuri hakuna majeruhi na maandalizi yanaendelea kwaajili ya mchezo wa mwingine wa kirafiki nchini Morocco ambapo watacheza na Gabon Aprili 22 na watarudiana tena kwa mchezo wa pili Aprili 25 mwaka huu na hii yote ni kuwaandaa vijana wetu na fainali hizo kwasababu" Amesema Alfred Lucas.
Katika hatua nyingine Shirikisho la Soka Barani Afrika, CAF limekiidhinisha kiwanja cha CCM Kirumba Jijini Mwanza kwa ajili ya kutumika kwa michuano ya Kimataifa baada ya ukaguzi kuonesha kuwa uwanja huo unakidhi vigezo
