Jumatano , 26th Jul , 2017

Nahodha wa Flying Dribblers, Geofrey Lea amefunguka kwa kudai upungufu wa wachezaji katika timu yake ndicho kilichosababisha wao kuchapwa pointi nyingi zaidi katika mchezo wa kwanza wa nusu fainali ya michuano ya Sprite BBall Kings

Nahodha wa Flying Dribblers, Geofrey Lea.

 mchezo umepigwa viwanja vya Don Bosco Oysterbay.

Lea amebainisha hayo muda mchache kumalizika kwa mechi hiyo ambayo ilitoka kwa pointi 116-67 dhidi Mchenga BBall Stars ambao mpaka sasa ndiyo timu pekee zilizokuwa zimewekea ushindani mkali wa piga nikupige kutokana na wachezaji wengi wa timu zote mbili kufahamiana vizuri uwezo wao wakiwa uwanjani.

"Flying Dribblers haiwezi kupotea kwa sababu hii ni 'game' ya kwanza pekee yake, kuna michezo mitatu, tunafasi nyingine mbili za kujiuliza na kuja kushinda. Kilichotukumba leo ni kutokana na uchache wetu tuliyokuwa nao, 'only seven player'walikuwepo kuna wachezaji watatu hawakuwepo kutokana na majukumu mbalimbali kwa hiyo game ijayo tuna uhakika tutashinda na ku-force 'game three' ambayo tuna nafasi ya kushinda pia", amesema Lea.

Pamoja na hayo, Lea amesema kitendo cha wachezaji wake kuingia katika matatizo ya kucheza vibaya ndicho kilichopelekea wao kushindwa kucheza deffence yenye uhakika zaidi mpaka kupelekea kufungwa pointi nyingi zaidi na wapinzani wao Mchenga BBall Stars.

Kwa upande mwingine, mechi ya pili ya ambayo itawakutanisha tena Flying Dribblers katika uwanja wa Don Bosco OysterBay Jijini Dar es Salaam, watakuwa wanakibarua kizito cha kusaka ushindi ili kusudi waweze kucheza 'game' ya tatu ambayo itaamulu ni nani aende katika hatua nyingine ya mwisho ya fainali za michuano hiyo.