French open yasogezwa mbele

Alhamisi , 8th Apr , 2021

Ufunguzi wa michuano ya tenisi ya wazi ya Ufaransa umeahirishwa kwa wiki moja ikiwa ni matumaini kwamba watazamaji zaidi wataruhusiwa kuhudhuria kushuhudia michuano hiyo.

Rafael Nadal akishangilia taji lake la michuano ya wazi ya Ufaransa alilotwaa mwaka jana.

Mashindano ya hayo ya Grand Slam huko Roland Garros sasa yataanza kutoka 30 Mei hadi 13 Juni na kufuzu wiki moja kabla.

Ufaransa iko katika kizuizi cha tatu kitaifa wakati wa kuongezeka kwa visa vya virusi vya Corona ambapo Rais wake Emmanuel Macron hapo awali alisema alitarajia kuwa kitamalizika katikati ya mwezi Mei mwaka huu.

Shirikisho la Tenisi la Ufaransa (FFT) limesema kuahirisha michuano hiyo ndio suluhisho bora.