Amani Simba katika moja ya michezo yake akiwa na Majimaji
Mkurugenzi wa Benchi la Ufundi wa African Lyon Charles Otieno amesema, wamepokea wachezaji wengi kutoka ndani na nje ya Tanzania lakini kwa sasa wanahitaji wachezaji wachache ambao wataweza kukiimarisha kikosi hicho.
Otieno amesema, wachezaji wanaowahitaji zaidi ni kwa upande wa magolikipa ambapo ndipo kuna mapungufu zaidi kwa sasa na wataungana na waliokuwemo ndani ya kikosi hicho.
Otieno amesema, wachezaji wapya walionao wameshawajaribu katika mechi za kirafiki na wameona uwezo wao hivyo wanaendelea kuyaangalia wale ambao watawahitaji kwa ajili ya kuanza nao kazi rasmi.
African Lyon
Katika hatua nyingine, kuna taarifa kuwa miongoni mwa wachezaji wanaowaniwa na timu hiyo ni golikipa mkngwe nchi Amani Simba ambaye alikuwa akiidakiwa Majimaji ya Songea.
Taarifa cha 'chini ya kapeti' zinaonesha kuwa golikipa huyo tayari yupo jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kumalizana na uongozi wa klabu hiyo.