"Nataka kusafiri kwenda Urusi bila wasiwasi sio tu kuhusu kujua nitakakocheza, lakini nataka kuwa na amani na utulivu wa akili kwamba nipo nilipo sasa sehemu nyingine'', amesema.
Kumekuwepo na tetesi za nyota huyo raia wa Ufaransa kutakiwa na vinara wa ligi kuu ya Hispania Barcelona na kauli yake hii imetafsiriwa kama shinikizo la kutaka mkataba mpya au kuruhusiwa kuondoka mwezi Juni.
Naye mshambuliaji wa Atletico Madrid ambaye amerejea kikosini akitokea Chelsea Diego Costa, amesema ana matumaini makubwa kuwa nyota huyo atasalia klabuni hapo na kuendelea kuitumikia timu yake.
Griezmann ambaye mkataba wake unamalizika tarehe 30 Juni mwaka 2022, kwasasa yupo kambini na timu ya taifa ya Ufaransa ambayo ijumaa itacheza na timu ya taifa ya Italia kwenye mchezo wa kalenda ya FIFA mwezi Machi.








