Haji Manara afunguka kuhusu kufukuzwa kazi Simba

Jumanne , 20th Aug , 2019

Msemaji wa klabu ya soka ya Simba Haji Manara amesema yeye bado ni msemaji wa Simba na hakuna kitu chochote, tofauti na inavyoelezwa mitandaoni kuwa amefukuzwa kazi.

Akiongea leo na wanahabari, Manara amesema kuwa mara nyingi vitu vingi vinaanzishwa mitandaoni na sio lazima yeye avitolee ufafanuzi lakini suala la kufukuzwa hajafukuzwa, japo ukweli ni kwamba hatokaa kwenye nafasi hiyo milele.

Aidha Manara amewataka mashabiki wa Simba kujitokeza kwa wingi uwanjani siku ya Jumapili kwenye mchezo wao wa marejeano dhidi ya UD Songo ya Msumbiji, utakaopigwa kwenye uwanja wa taifa.

Zaidi tazama Video hapo chini