Jumapili , 9th Apr , 2017

Dereva wa Mercedes Lewis Hamilton ambaye ametawala katika mashindano ya Chinese Grand Prix amefanikiwa kuchukua taji lake la kwanza kwa mwaka huu, baada ya kumshinda Dereva wa Ferrari Sebastian Vettel.

Mpambano huo ulikuwa unawapa nafasi wababe wote waliofika mwisho yaani Hamilton na Vattel lakini umakini wa uendeshaji wa Hamilton ulimpa ushindi Muingereza huyo.

Madereva hao, kwa jinsi walivyokuwa wakichuana inatoa ishara jinsi gani mwaka huu, wanaweza kuwa na upinzani mkali kwa timu zao za Mercedes na Ferrari.

Dereva wa Red Bull Max Verstappen alitoka nafasi ya 16 na kumaliza akiwa nafasi ya tatu.