Wallace Karia Rais wa TFF anaetetea nafasi yake na mgombea pekee wa nafasi ya urais aliyepitishwa na kamati ya uchaguzi
Hii ni baada ya mawakili wa pande zote mbili kuwasilisha hoja zao mbele ya jaji na sasa itakuwa ni kutoa hukumu ndogo ya ama kuzuia uchaguzi wa TFF au kusimamishwa.
Hapo jana Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Dar es Salaam ilitangaza kupokea kesi ya kupinga uchaguzi wa Shirikisho la Soka nchini (TFF) na taarifa ya Mahakana ilieleza kuwa imemtaka Rais wa TFF Wallace Karia, Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi na Bodi ya Wadhamini wa Shirikisho hilo kufika Mahakamani leo Julai 3, 2021 kujibu hoja za kwa nini uchaguzi wa TFF usisimamishwe.
Uchaguzi wa viongozi wa TFF umepangwa kufanyika mkoani Tanga Agosti 7, 2021. Lakini kueleka katika uchaguzi huo nafasi ya Urais amebaki mgombea mmoja tu Wallace Karia ambae ndio Rais wa sasa baada ya wagombea wengine kuenguliwa kwa kukosa sifa za kuendalea na mchakato wa Uchaguzi, nafasi nyingine zinazogombaniwa ni nafasi za wajumbe sita wa kamati ya utendaji ya TFF.



