
Katika droo ya leo kuna uwezekano mabingwa watetezi Bayern Munich kupangwa dhidi ya FC Barcelona
Timu 8 zilizomaliza vinara wa makundi zitapangiwa kucheza na timu 8 zilizomaliza nafasi ya pili kwenye hatua hiyo iliyopita.
Timu zilizomaliza vinara wa makundi kutoka Ujerumani ni Bayern Munich ambao ni mabingwa watetezi wa michuano hii na Borussia Dortmund, mabingwa mara 13 na wa kihistoria wa michuano hii Real Madrid nao wapo kutoka Hispania, Manchester City, Chelsea na mabingwa mara 6 Liverpool zinawakilisha England, Juventus ya Italia na PSG ya Ufaransa.
Zile zilizomaliza nafasi ya pili kwenye hatua ya makundi ni Atletico Madrid, Sevilla na FC Barcelona za Hispania, Atalanta, Lazio za italia, kutoka Ujerumani ni Leipzig na Borussia Mönchengladbach, huku FC Porto ikiiwakilisha Ureno.
Katika hatua hii timu zilizomaliza vinara wa makundi zitaanzia ugenini na kupata faida ya kumalizia mchezo wa pili nyumbani, lakini pia timu zilizokuwa kundi moja na zile zinazotoka nchi moja kikanuni haziruhusiwi kukutana katika hatua hii ya 16 bora.
Michezo ya mkondo wa kwanza itachezwa tarehe 16/17/23/24 Februari na ile ya mkondo wa pili itachezwa tarehe 9/10/16/17 mwezi Machi.