Kinda wa Ujerumani Kai Haverts (Pichani) anawania na vilabu vikubwa Barani Ulaya.
Inaripotiwa kuwa kocha wa The Blues ,Frank Lampard amezungumza na kiungo huyo raia wa Ujerumani juu ya kumuhitaji kwenye kikosi chake msimu ujao hivyo Chelsea wanakaribia kukamilisha makubaliano binafsi na mchezaji kabla ya kumalizana na klabu yake.
Chelsea wanapewa kipaumbele zaidi kuinasa saini ya Haverts kwa sababu ndio timu pekee iliyoonyesha nia ya kulipa pauni million 73 kama ada ya uhamisho, licha ya vilabu vya Real Madrid na Bayern Munich kuonyesha nia ya kuhitaji huduma ya kiungo huyo.
Havertz ana umri wa miaka 21 amekuwa na kiwango bora msimu huu akiwa na kikosi cha Bayer Leverkusen, amefunga mabao 17 na ametoa pasi za usaidizi wa magoli 8 katika michuano yote akiwa amecheza jumla ya michezo 43 msimu huu.



