Jumanne , 6th Jun , 2017

Droo ya pili ya kupanga ratiba ya michuano ya kikapu ya 'Sprite Bball Kings' imefanyika usiku wa kuamkia leo Jijini Dar es salaam kwa usimamizi wa Shirikisho la mpira wa kikapu Tanzania {TBF} kushirikiana na EATV LTD na kushuhudiwa na timu shiriki.

Meneja Masoko na Mauzo kutoka East Africa Television LTD, Roy Mbowe (Kulia) akiwa na Kamisaa kutoka FIBA, Wiliam Guard Mziray

Michuano hiyo itakayoshirikisha timu 18 ambazo ziliweza kufuzu hatua ya awali na kuanza kutimua vumbi siku ya Jumamosi Juni 10 katika uwanja wa Airwing uliopo Ukonga Jijini Dar es salaam.
Akizungumza wakati wa zoezi hilo, Mwakilishi kutoka Shirikisho la Mpira wa Kikapu Tanzania - Tanzania Basketball Federation (TBF), Mwenze Kabinda amewataka wachezaji hao waache nidhamu ya uoga wa kuhofia timu pinzani waliopangiwa nayo na kupelekea kuingia mitini siku ya tukio.
"Haya mashindano lengo lake ni kuibua vipaji kwa vijana pamoja na kurudisha heshima ya mpira wa kikapu. Hivyo napenda watu waje washindane msitegemee 'walkover' maana mnarudisha nyuma mchezo pamoja na kuwavunja moyo wadhamini wa mashindano haya" alisema Kabinda

Naye Meneja Masoko na Mauzo kutoka East Africa Television LTD, Roy Mbowe amewasisitizia waakilishi waliojitokeza kushuhudia droo hiyo wazingatie masharti na vigezo vyote vilivyoweka kwenye mashindano.

                Wawakilishi wa timu mbalimbali waliohudhuria kushuhudia droo ya wazi ya Pili michuano ya Sprite Bball Kings

MATOKEO YA DROO

Hii ndiyo ratiba kamili ya michuano ya Sprite Bball Kings itakayoanza kutikisa siku ya Jumamosi ya Juni 10 katika uwanja wa Air wing, Ukonga Jijini Dar es Salaam kwa mechi nane za kwanza.