Jumatano , 21st Feb , 2018

Nyota wa zamani wa Arsenal Thierry Henry amesema anaamini Neymar hawezi kukimbia kivuli cha Lionel Messi labda abadaili aina ya mchezo lakini si kuhama timu na kuendelea kucheza soka.

"Sijui kama Neymar alitoka Barcelona kukimbia kivuli cha Messi, ni kweli kwamba wachezaji wote wako katika kivuli cha Messi, na kama Neymar hataki kuwa, anapaswa kubadili mchezo," amesema Henry.

Neymar alishangaza dunia ya wapenda soka kwenye dirisha la usajili la mwezi nJuni 2017 baada ya kukubali dau la rekodi ya dunia € 222 millioni zaidi ya shilingi bilioni 600 akitoka Barcelona na kutua Paris Saint-Germain.

Neymar amekuwa na mwanzo mzuri ndani ya PSG, akifunga mabao 28 katika mechi 29 kwenye mashindano yote ambayo yameisaidia timu yake kuongoza ligi mbela ya Monaco.