Mshambuliaji wa Aston Villa ambaye pia ni nahodha wa Taifa Stars Mbwana Samatta (Pichani) akishangilia bao aliloifungia klabu yake.
Tayari Norwich City wameondoka na Villa wanapambana na Watford, Westham United na AFC Bournermouth kukaa nafasi ya 17 ili wasishuke daraja.
Matokeo mabovu ya Watford katika mechi zao mbili zijazo na matokeo chanya ya Aston Villa katika mechi zao mbili za mwisho ndio namna pekee ya Mbwana Samatta kubaki EPL,kwa kifupi ni kwamba wa kuwaokoa Aston Villa ni Villa wenyewe na si vinginevyo.
Villa wanashikilia nafasi ya 18 wakiwa na alama 31 baada ya kushuka dimbani mara 36,alama hizo ni sawa na Bournemouth walioko nafasi ya 19 lakini wao tayari wameshacheza michezo 37.
Vinaja wa kocha Dean Smith , Villa wana mechi na Arsenal hii leo na kisha watamalizia na Westham United.
Michezo hii yote watatakiwa kuondoka na alama walau 4 huku wakiomba dua wapinzani wao wapoteze michezo yao iliyobaki.
Wakipata alama 4 katika mechi hizi mbili ina maana watafikisha alama 35 na kama Watford watapoteza mechi zao mbili zilizobaki ambazo ni ngumu sana(vs Man City & vs Arsenal) ina maana watabaki na alama 34 hivyo Villa watakwea hadi nafasi ya 17 na Watford atarudi 18.
Vipi wakipoteza mechi zote au wakasuluhu? Hapo ni kushuka daraja tu, maana wakisuluhu mechi mbili ni alama mbili ina maana watafikisha alama 33, wakifungwa zote watabaki na 31.
VILA ITASHUKA?
Kweli,Villa itashuka daraja iwapo tu Watford itaifunga Manchester City katika mchezo wa usiku wa leo.
TAKWIMU MUHIMU .
-Aston Villa imepoteza mechi 6 mfululizo za EPL dhidi ya Arsenal kwa kuruhusu mabao 19 huku wao wakifunga mabao matatu tu.
-Villa haijashinda katika mechi 17 mfululizo za mwisho katika EPL ikiwa nyumbani kwake,Sare 7 na vipigo 10.
-Arsenal haijafungwa katika michezo 18 kati ya 20 dhidi ya timu zilizo chini ya 10 bora kwenye msimamo wa EPL,imeshinda 10 na sare 8 huku ikifungwa mara 2.
-Iwapo Arsenal itakosa ushindi leo,itakua imeshinda michezo minne tu ya ugenini katika msimu huu na itakua ndiyo rekodi kwa klabu yao.





