Jumanne , 26th Jan , 2021

Wenyeji wa michuano ya CHAN timu ya taifa a Cameroon itaminyana na timu ya taifa ya Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo kwenye mchezo wa robo fainali ya fainali hizo, wakati Mali wataminyana na Congo kwenye mchezo mwingine wa robo fainali. Michezo hii itachezwa Januari 30.

Wenyeji Cameroon wataminyana na timu ya taifa ya DR Congo kwenye mchezo wa robo fainali ya michuano ya CHAN

Congo DR na Congo zimekata tiketi kwa kucheza robo fainali baada ya kushinda michezo yao ya mwisho kwenye michezo ya kundi B jana usiku, Congo DR waliifunga Niger mabao 2-1, ushindi ambao imekifanya kikosi hicho kumaliza vinara wa kundi hilo wakiwa na alama 7, na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Libya ulitosha kuifanya Congo kumaliza nafasi ya pili wakiwa na alama 4.

Wenyeji Cameroon walifuzu hatua ya robo fainali baada ya kumaliza nafasi ya pili kwenye msimamo wa kundi A wakiwa na alama 5, baada ya kushinda mchezo 1 na kutoka sare michezo 2, na wataminyana na vinara wa kundi B timu ya taifa ya DR Congo, Vinara wa Kundi A Mali ambao walimaliza wakiwa na alama 7 watacheza dhidi ya Congo washindi wa pili wa kundi B, kwenye mchezo wa robo fainali.

Michezo yote hii itachezwa Januari 31, mchezo wa Mali dhidi ya Congo utachezwa mjini Yaounde, na mjini Douala utachezwa mchezo kati ya DR Congo na Cameroon.

Michuano hiyo itaendelea tena leo kwa michezo 2 ya kundi C, ambapo Uganda wanaoburuza mkia kwenye kundi hilo wakiwa na alama 1 watacheza dhidi ya vinara Morocco wenye alama 4, Togo wanaoshika nafasi ya pili kwenye kundi wakiwa na alama 3 watacheza dhidi ya Rwanda wanaoshika nafasi ya 3 wenye alama 2.