
Wazir Junior
Waziri Jr amesema hayo leo Agosti 24, 2021 kwenye Kipenga Xtra ya East Africa Radio inayosikika Jumatatu mpaka Ijumaa kuanzia saa 6:00 hadi 7:00 mchana.
''Ndani ya mechi 9 za kwanza nikiwa Yanga sikucheza, nilikuja kupata bahati kucheza mechi ya 10 ambayo ilikuwa dhidi ya KMC na ndio maana nikamwambia Makapu kuwa naenda kufunga leo na nikaandika ujumbe ule wa ''Mwamba wa CCM Kirumba'' na kweli nikafunga'' - Wazir Junior
Aidha Wazir Junior ameongeza kuwa, ''Changamoto kubwa ya vilabu vyetu ni kukosa watu wa saikolojia labda mpaka kocha aongee na wewe. Nashukuru kocha Nasreddine Nabi kwenye mechi ya Yanga Vs Simba SC aliniambia sababu za kutocheza na kesho yake nilikuwa wa kwanza kufika mazoezini'' - Wazir Junior.
Tazama video hapo chini