Jumatano , 30th Jan , 2019

Klabu ya soka ya Simba imeweka wazi kuwa ipo kwenye hatua za mwisho kukamilisha dili la mchezaji wake winga Shiza Kichuya kwenda kwenye klabu ya Pharco ya Misri.

Shiza Kichuya

Simba imethibitisha hilo kupitia taarifa yake kwa umma ambapo imeweka wazi kuwa muda wowote kuanzia sasa itamalizana na Pharco.

Ifahamu zaidi Pharco

Pharco inashiriki ligi daraja la pili nchini humo ambayo ni ya pili kwa ngazi ya ubora ukiacha ligi kuu ambayo hujulikana kama ligi daraja la kwanza.

Makao makuu ya Pharco ambayo ilianzishwa mwaka 2010 yapo jijini Alexandria na Mwenyekiti wake ni Ezz Bashar Helmy.

WATANZANIA MISRI
Kichuya anakwenda kuwa mchezaji wa 3 wa Tanzania anayecheza Misri wengine wakiwa ni Himid Mao na Yahya Zayd.