Jumamosi , 12th Oct , 2019

Balozi wa Tanzania nchini Rwanda IGP Mstaafu Balozi Ernest Jumbe Mangu, ameeleza umuhimu wa mchezo wa kirafiki kati ya Tanzania dhidi ya Rwanda utakaopigwa Oktoba 14, 2019, ambapo amewataka wachezaji kucheza kama mechi ya mashindano.

Wachezaji wa Taifa Stars wakifanya mazoezi

Balozi Mangu amesema, kwa kuwa mchezo huo ni wa maandalizi ya mchezo wa marudiano kufuzu CHAN dhidi ya Sudan Oktoba 18, 2019, wachezaji wanatakiwa kuutumia vizuri ili waweze kushinda mechi ijayo.

'Karibuni sana Rwanda, mujiandae vizuri nafikiri mnaendelea kufanya mazoezi kwaajili ya mchezo huu wa Jumatatu, mchezo huu ni muhimu sana sio kwenu tu hata kwa taifa kwa ujumla', amesema Balozi Mangu.

Kikosi cha Taifa Stars kiliwasili nchini Rwanda jana, tayari kwa mchezo wa kirafiki wa kalenda ya FIFA, ambapo baada ya mchezo huo itaunganisha kwenda Sudan, kucheza mchezo wa marudiano kuwania kufuzu CHAN.