
Hersi Said amechukua fomu kugombea nafasi ya Urais wa Yanga
Mkurugenzi wa uwekezaji wa GSM, Injinia Hersi jana alichukuliwa fomu ya kugombea Urais wa klabu hiyo katika uchaguzi utakaofanyika mwezi Julai na wazee wa klabu hiyo.
Leo wazee wa Klabu ya Yanga wamerudisha fomu hiyo ikiwa imejazwa tayari kwa kuanza mbio za Urais wa Klabu hiyo.
Mwakalebela amesema kuwa Yanga wanatambua namna Injinia alivyokuwa akijitoa kwa ajili ya timu hiyo inayoshiriki Ligi Kuu Bara.