Wachezaji wa timu ya Taifa ya Italia wakishangilia kwenye moja ya michezo ya Euro 2020
Kocha wa Hispania, Luis Enrique amesema Italia hii ya sasa tofauti na ya zamani kwani nayo inauwezo mkubwa wa kumiliki mpira na wanafafana namna wanavyocheza hivyo anaamini vita kubwa itakuwa kwenye timu ipi itamliki mpira zaidi,wakati kocha wa Italia Roberto Mancini amesema lazima waonyeshe kiwango bora kwenye mchezo huu kwa sababu wanacheza na timu bora.
Huu utakuwa mchezo wa 10 timu hizi kukutana kwenye mashindano makubwa kombe la Dunia na michuano ya Euro na zitaweka rekodi ya kuwa timu zilizokutana mara nyingi zaidi kwenye michuano mikubwa ambapo Kwenye michezo tisa iliyopita Italia imeshinda michezo 4 Hispania imeshinda mchezo mmoja na sare michezo 4.




