Mkono ukiwa umegongelewa na msumari
Imeelezwa kuwa wakazi wa kaunti ya Vihiga Magharibi mwa Kenya walipigwa na butwaa baada ya kumuona kijana mwenye umri wa miaka 19 ambaye mikono yake ilikuwa imepigiliwa misumari kwenye mti kwa madai kuwa ni mwizi wa redio.
Kwa mujibu wa taarifa ya polisi imeelezwa kwamba kijana huyo alikutwa mikono yake miwili ikiwa imewekwa kwenye tawi la mti na kupigiliwa misumari, baada ya kupokea taarifa kutoka kwa kiongozi wa North Izava, akiwaeleza kuhusu tukio hilo





