.jpg?itok=Pqb0Jk-M×tamp=1630325038)
Jake Paul (Kulia) akimtwanga ngumi mpinzani wake Tryone Woodley.
Waamuzi wawili kati ya watatu wa pambano hilo walitoa uamuzi wa faida ya ushindi kwa Paul wa alama 77-75, 78-74, huku Mwamuzi mmoja akimpa Woodley alama 77-75.
Hata hivyo Woodley hakuoneshwa kuridhishwa na uamuzi huo uliotolewa na waamuzi hao ambao ulimfaidisha mpinzani wake Paul, huku akisema anatarajia wawili hao warudiane katika pambano lingine ambalo litamaliza ubishi kati ya wababe hao.
Paul ambaye anafikiwa kufikisha rekodi ya kucheza mapambano manne bila kupoteza, huku pambano lake la kwanza likiwa dhidi ya Ali Eso Gib, lifikuatiwa dhidi ya mchezaji wa zamani kikapu wa ligi ya Marekani maarafu kama NBA, aitwaye Nate Robinson na baadaye kumpiga mpiganaji wa zamani wa UFC Ben Askren.