Ijumaa , 25th Jan , 2019

Mwanamuziki mkongwe wa Bongo Fleva, mwanadada Lady Jay Dee amefunguka namna alivyopata ofa  kurekodi wimbo wake wa kwanza ambao ulimfungulia njia ya mafanikio yake hadi hivi sasa.

Lady Jay Dee

Kupitia ukurasa wake wa Twitter, Jay Dee amesema kuwa kutokana na kutokuwa na pesa ya kurekodi wimbo wake katika studio za MJ Records, alipata ofa ya kurekodi wimbo baada ya kushinda shindano la vipaji halisi.

Shindano hilo lilikuwa likirushwa na Radio One Stereo, ambapo kwa kipindi hicho mtu alikuwa akipigiwa simu na kisha ku'rap' au kuimba ili kuonesha kipaji chake.

Lady Jay Dee amefanikiwa kudumu katika muziki wa Bongo Fleva kwa miaka takribani 20, akidumu na ufundi wake ule ule. Ametoa jumla ya albamu 7 mpaka sasa, ambazo ni Machozi (2000), Binti (2003), Moto (2005), Shukrani (2007), The Best of Lady Jaydee (2012), Nothing But The Truth (2013) pamoja na Woman (2017).