Jumatatu , 31st Mei , 2021

Mbunge wa Makete, Festo Sanga, ameishauri serikali kujenga 'Sports Arena' ambayo itasaidia hata Rais atakapokuwa akitaka kuzungumza na wananchi aitumie bila kuathiriwa na mvua ama hali ya hewa yoyote kwa sababu mara nyingi matukio makubwa yamekuwa yakifanyika kwenye viwanja vya wazi.

Mbunge wa Makete, Festo Sanga

Kauli hiyo ameitoa hii leo Mei 31, 2021, Bungeni Dodoma, wakati akichangia hotuba ya Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, iliyowasilishwa Bungeni hapo na Waziri wake Innocent Bashungwa.

"Nchi hii bila Arena ni ukoloni, Dar es Salaam tunahitaji Sports Arena ya watu 50,000 au 60,000, Rais akitaka kuongea na Taifa hili ni uwanja wa Taifa mvua ikinyesha watu wanaanza kukimbia, tafuteni Arena ambayo Rais akitaka kuongea watu mnaingia mle ndani, iandikeni hata JPM Arena au Samia Arena halafu Watanzania watawakumbuka," Mbunge Sanga. amesema Mbunge Sanga.