
Nyota wa Philadelphia 76ers, Joel Embiid.
Baada ya kusaini mkataba mpya, Embiid ambaye alishika nafasi ya pili kwenye kuwania tuzo ya mchezaji bora wa NBA nyuma ya Nicola Jokic wa Denver Nuggets, amesema hakuna sehemu nzuri ya kuwepo zaidi ya kuwa Philadelphia na sasa yupo tayari kuwania ubingwa wa NBA msimu ujao.
Mkabata wa Embiid unatahamani ya dola za kimarekani milioni 196 sawa na bilioni 454 na zaidi ya milioni 500 za kitanzania na kumfanya awe mchezaji wanne mwenye mkataba mnono kwenye NBA kwa sasa huku nafasi ya kwanza ikishikiliwa na Stephen Curry wa Golden State Warriors mwenye mkataba wa thamani ya milioni 215 dola za kimarekani sawa na zaidi ya bilioni 498 za kitanzania.