
Kocha wa Tottenham Hotspurs, Jose Mourinho akishangilia.
Kuelekea kwenye mchezo huo, Spurs watawakosa Erick Lamela anayetumikia adhabu baada ya kuvunja utaratibu unaomtaka kukwepa muingiliano isiyo na ulazima kama tahadhari ya COVID-19, Giovani lo Celso na Gareth Bale wanaoendelea kuwa nje ya uwanja kutokana na majeraha yao.
Kwa upande wa Brentford, vijana wa kocha Thomas Frank wanatazamiwa kumkosa mchezaji mmoja pekee Shandon Baptiste, ilhali wengine wakiwa fiti kuwavaa masharabaro hao wajiji la londo klabu ya Spurs.
Mchezo huo ndiyo fursa pekee iliyokuja kwa haraka kwa kocha Jose Mourinho kuandika historia ya kutinga fainali ya kwanza tokea achaguliwe kuwa kocha wa Spurs Novemba 20 mwaka jana kuchukua mikoba ya Mauricio Pochettino aliyetimkia PSG siku chache zilizopita.
Mourinho kama atafanikiwa kutinga fainali ya mchezo huo basi ataweka rekodi ya kutinga fainali mara 5 huku akiwa na rekodi ya kibabe ya kutwaa kombe hilo mara zote nne alizotinga fainali akiwa na vilabu vya Chelsea na Manchester United.
Brentford wametinga hatua hiyo ya nusu fainali ikiwa ni kwa mara yao ya kwanza kutinga nusu fainali kwenye michuano hiyo tokea klabu hiyo ianzishwe miaka 131 iliyopita.
Kocha wa Brentford Thomas Frank akiwapongeza wachezaji wake baada ya kuwafunga Newcastle na kutinga nusu fainali ya Carabo Cup kwa mara ya kwanza.
Rekodi zinaonesha wawili hao tayari wameshakutana mara 3 kwenye kombe hilo na Spurs kushinda michezo yote 3 na kuendeleza ubabe wa kumfunga Brentford michezo 5 na kutoka sare 2 kwenye michezo yote 7 ambayo wamekutana kwenye michuano yote.
Hii ni mara ya 16 Spurs inatinga hatua ya nusu fainali ya kombe la Carabao na kufanikiwa kutinga fainali mara 8 na kufanikiwa kutwaa taji hilo mara 4 mara ya mwisho ikiwa mwaka 2008 ambapo waliifunga Chelsea huku uwanja wa Wembley ukitumika kwa mara ya kwanza kwenye Carabao.