Jumanne , 4th Aug , 2020

Aliyewahi kuwa Kocha na Mchezaji wa klabu ya Simba, Jamhuri Kihwelu ''Julio'' amesema ni mufa muafaka kwa Viongozi na wapenzi wa Simba, kujua umuhimu wa kutoa muda kwa Mwalimu wao na Kocha kwakuwa matunda yake huwa yanaonekana iwapo watakuwa wavumilivu.

Kocha Mkuu wa Klabu ya Simba, Sven VanDenbroeck (Kulia pichani), akiwa na msaidizi wake Seleman Matola (Kushoto) wakijadili jambo mazoezini.

Kauli ya Julio aliiotoa kwenye mazungumzo yake na Mtaalam wa soka kutoka East Africa Television, Ibrahim Kasuga ambaye  alimuuliza juu ya kiwango cha Sven na hata wachezaji ndani ya msimu uliomalizika wiki iliyopita.

Julio alisema, ''Hata nilipokuja katika Kipindi chenu cha Kipenga Xtra, nilisema kocha huyu ana kitu, apewe muda, hata takwimu zake zinaonyesha ana kitu, pia tazama alivyobadilisha wachezaji, ni kweli nyota wa Simba wengi umri umesogea, wanahitaji kupata muda kutoka mechi moja hadi nyingine, wakicheza mfululizo hawa wanachoka,Je mtaalam hujaliona katika fainali ya FA?''

Julio akaongeza ''nilimzungumzia Gerson Fraga, wengi walisema hakuna Mbrazil anayecheza soka Tanzania, lakini nyote mmeshuhudia huyu wa Simba anachokifanya''.

Kocha huyo anayesifika kwa kuongea ukweli, amesema kwa alichokifanya Sven haoni sababu ya Viongozi kumfuta kazi bali aongezewe rasilimali zitakazomuwezesha kufanya vizuri zaidi, na ameongeza kuwa iwapo watamtimua atawashangaa na hatowaelewa.