Ijumaa , 26th Nov , 2021

Kiungo wa zamani wa Yanga, Thaban Scara Kamusoko (33) amefunguka na kuwatahadharisha watani wake wa jadi klabu ya Simba isiwachukulie poa Red Arrows maana pia ni timu nzuri.

(Thaban Kamusoko alipokuwa Yanga)

Kamusoko ameyasema hayo zikiwa zimesalia siku tatu kuelekea kwenye mchezo huo utakaochezwa Novemba 28, 2021 ukiwa ni wa mkondo wa kwanza wa mtoano kuwania kufuzu makundi michuano ya kombe la Shirikisho Afrika.

Nyota huyo amesema  "Siyo timu ya kutisha. Lakini imacheza kitimu zaidi na inabadilisha mfumo kulingana na timu inayocheza nayo. Ina straika wao (Chamanga) ndiye wanamtegemea sana kuwafungia mabao"

Ikumbukwe kuwa, Thaban Scara Kamusoko aliichezea Yanga mwaka 2015 hadi 2019 kwa mafanikio makubwa ikiwemo kutwaa mataji ya ligi kuu mawili ya Ligi kuu, moja la FA na kucheza makundi ya michuano ya kombe la Shirikisho Afrika.