Jumatano , 8th Jun , 2022

Mshambuliaji wa England Harry Kane amefikisha bao lake la 50 baada ya kuisawazishia England kwenye sare ya bao 1-1 dhidi ya Ujerumani kwenye mchezo wa Uefa Nations League wa kundi A 3 uliofanyika kwenye uwanja wa Allianz Arena nchini Ujerumani usiku wa jana.

(Harry Kane na akishangilia baada ya kufunga goli dhidi ya Ujerumani)

Nahodha huyo wa England mwenye miaka 28 alifunga bao hilo kwa mkwaju wa penalti dakika ya 88 na kumpiku gwiji wa zamani wa England Sir Bobby Charlton mwenye magoli 49 huku akizidiwa na kinara wa ufungaji ndani ya England Wayne Mark Rooney mwenye magoli 53

"Magoli 50 ndani ya England ni jambo la kujivunia sana kwangu na kwa kila mtu, maana haijaja kama zawadi ila jambo la muhimu ni kupata alama moja muhimu ugenini dhidi ya timu ngumu. Tuendelee kupambana zaidi" ameandika Kane kwenye ukurasa wake wa Instagram.

England inakamata nafasi ya mwisho kwenye League A wakiwa na alama 1 baada ya Jumamosi iliyopita kupoteza mbele ya Hungary kwa kichapo cha bao 1-0 huku matokeo mengine ya kundi ,Italia walichomoza na ushindi wa magoli 2-1 dhidi ya Hungary.