
Ng'olo Kante (kushoto) na Eden Hazard (kulia)
Kante mwenye umri wa miaka 27 ni miongoni mwa wachezaji waliowaniwa kwa nguvu na vigogo wa ligi ya Ufaransa, PSG msimu uliopita, ambapo sasa ofa hiyo itafifisha matumaini ya PSG kumnasa mchezaji huyo.
Kwenye ofa hiyo, Chelsea imepanga kumpa mshahara wa Pauni 290,000 kwa wiki ambazo ni sawa na takribani Sh milioni 853 za kitanzania, mshahara ambao utamfanya kuwa mchezaji anayelipwa zaidi klabuni hapo akimzidi nyota wa klabu hiyo kwa sasa, Eden Hazard anayelipwa Pauni 200,000 kwa wiki.
Hazard amekuwa kwenye rada za Real Madrid kwa muda mrefu hivi sasa na yeye mwenyewe aliwahi kueleza kuwa ana ndoto za kuja kucheza katika ligi kuu ya Hispania 'La Liga', jambo ambalo linazidisha matumaini ya vigogo hao kuweza kumnyakua muda wowote.
Ni wazi kuwa dili la mkataba mpya wa Kante likikasmilika litaamsha vuguvugu la wachezaji wengine mastaa klabuni hapo wakiwemo Eden Hazard na Willian kutaka mikataba mipya ama kuachana na klabu hiyo.
Bosi mpya wa Chelsea, Maurizio Sarri ana malengo ya kuendelea kuwabakiza mastaa wake hasa baada ya kushindwa kumzuia, Thibaut Courtois kujiunga na Real Madrid mwanzoni mwa msimu huu.