Jumapili , 8th Mei , 2022

Bingwa wa ngumi na mateke (Kick Boxing) Tanzania, Japhet Kaseba, ameshinda nafasi ya Mwenyekiti wa chama cha mabondia wa ngumi za kulipwa Tanzania (TPBA) kwenye uchaguzi wa chama hicho uliofanyika mapema leo.

Mwenyekiti wa kwanza wa TPBA, Japhet Kaseba(pichani)

Kaseba anakuwa mwenyekiti wa kwanza wa chama hicho, akipata kura za ndio 26 na kumshinda mpinzani wake Mada Maugo aliyepata kura za ndio 16.

Nafasi ya Katibu Mkuu imeenda kwa Slum Mgeni aliyepata kura 36, wajumbe wawili ni Francis Miyeyusho aliyepata kura 24 na Fatuma Yazidu aliyepata kura 25. naye Dullah Mbabe akiangukia katika nafasi ya ujumbe kwa kupata kura 20.