
Kikosi cha timu ya Simba
Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo nchini Tanzania imesema katiba ya klabu ya Simba iliyopelekwa na uongozi wa klabu hiyo imeshapitiwa na kubainika kuwa na kasoro ndogo zinazoweza kurekebishwa ndani ya muda mfupi tayari kuelekea katika uchaguzi mkuu wa klabu hiyo.
Akiongea jijini Dar es salaam, Mkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo wa wizara hiyo, Leonald Thadeo, amesema kinachosubiriwa kwa sasa ni kuikabidhi katiba hiyo kwa uongozi wa klabu hiyo kwa ajili kufanya marekebisho madogo ili kuisajili katiba hiyo.