Alhamisi , 28th Apr , 2022

Mwamuzi Ramadhan Kayoko, ameteuliwa kuwa msimamizi wa Sheria 17 za mchezo wa NBC Premier league kati ya wenyeji Yanga SC dhidi ya Simba SC siku ya Jumamosi katika dimba la Benjamin Mkapa.

Kayoko ametajwa na TFF baada ya kuwepo kwa tetesi kuwa angechezesha pambano hilo linalosubiriwa kwa hamu kubwa na mashabiki wa soka la Bongo na kwingineko Barani Afrika.

Mwamuzi huyo kutoka Dar es salaam, atasaidiwa na Frank Komba wa Dar es salaam na Mohamed Mkono kutoka Tanga, huku Nassoro Hamduni kutoka Kigoma akitajwa kuwa mtathimini wa waamuzi na Isaack Munis kutoka Kilimanjaro atakua Kamishna wa mchezo.

Kabla ya mchezo huo Kayoko pia alichezesha mchezo wa Nusu Fainali Kombe la Shirikisho Tanzania Bara ‘ASFC’ mwaka 2020, Uwanja wa Benjamin Dar es salaam.

Mchezo huo ulimalizika kwa Young Africans kukubali kichapo cha mabao 4-1.