Kikosi cha mwisho Stars kuelekea AFCON chatajwa

Jumatano , 12th Jun , 2019

Kocha wa timu ya taifa ya Tanzania 'Taifa Stars', Emanuel Amunike ametangaza kikosi cha wachezaji 23 ambao wataiwakilisha Tanzania katika mmichuano ya AFCON.

Taifa Stars

Kikosi hicho kilichopo nchini Misri kujiandaa na maandalizi ya mwisho kwaajili ya michuano hiyo, kiliondoka nchini na wachezaji 32 ambapo wachezaji 9 ndiyo waliotemwa.

Wachezaji waliotemwa ni pamoja na  Shaban Chilunda, Miraji Athumani, Abdi Banda, Shiza Kichuya, David Mwantika, Selemani, Tangalu pamoja na makinda Kelvin John na Bonifase- Golikipa wa U18.

Kikosi kilichotangazwa ni kama kinavyoonekana hapo chini.