(Kocha Thomas Tuchel wa Chelsea na Jurgen Klopp wa Liverpool)
Upande wa Makocha Thomas Tuchel na Jurgen Klopp wote wameshawahi kutwaa mataji ya Ulaya pamoja na timu zao, lakini hakuna hata mmoja aliyeshinda kombe la ndani katika soka la Uingereza. Chelsea ilishinda taji hilo mara ya mwisho mwaka 2015, lakini kwa Liverpool ni takribani miaka 10 imepita tangu ilipotwaa taji hilo.
Mabingwa watetezi wa kombe hilo Manchester City ambao walishinda taji hilo kwa miaka minne iliyopita, ambapo fainali ya mwaka 2019 waliwafunga Chelsea kwa mikwaju ya penalti, msimu huu walitupwa nje katika raundi ya nne na West Ham United.
(Kombe la ligi - Carabao Cup)
Hili ni taji la kwanza kati ya mataji manne ambayo Liverpool wanaweza kushinda msimu huu, baada ya kupunguza toafuti ya alama na Manchester City wanaoongoza katika msimamo wa ligi kuu ya England kwa tofauti ya alama tatu na pia bado wapo katika kinyang'anyiro cha Kombe la FA.
Na kwa upande wa mabingwa watetezi wa Ligi ya Mabingwa ulaya, Chelsea wao wanaweza kukamilisha taji lao la tatu la msimu huu mapema kama watashinda mchezo wa leo, kwani tayari wameshabeba taji la Super Cup la Uropa na Kombe la Dunia kwa ngazi ya vilabu mwaka huu.

