Jumatatu , 9th Mar , 2020

Kocha Mkuu wa Aston Villa, Dean Smith amezungumzia juu ya kiwango cha Samatta tangu alipojiunga na klabu hiyo kwenye dirisha dogo la usajili la Januari mwaka huu.

Kocha wa Aston Villa na Mbwana Samatta

Akizungumza na mtandao wa klabu hiyo kuelekea katika mchezo wa leo wa Ligi Kuu ya Uingereza (EPL) dhidi ya Leicester City, Smith amemtaja Samatta kuwa ni kijana mwenye akili kubwa ambaye ataisaidia klabu hiyo katika wakati huu.

"Samatta anakubalika, mchezaji mwenye akili na ambaye anaweza kuwa msaada mkubwa kwa timu katika kipindi hiki hadi mwishoni mwa msimu", amesema kocha huyo.

Pia amesema kuwa muunganiko wa Samatta pamoja na wachezaji wengine kama Marvelous Nakamba {Mzambia}, John McGinn, Jack Grealish na Tyrone Mings na kusisitiza kuwa wakicheza kama walivyocheza dhidi ya Manchester City katika fainali ya Kombe la Ligi, watakuwa na nafasi kubwa zaidi ya kufanya vizuri.

Aston Villa ipo katika nafasi ya 19 ya msimamo wa EPL ikiwa na pointi 25, ambapo ikifanikiwa kushinda mchezo dhidi ya Leicester City itapanda hadi nafasi ya 16.