
Kocha Zdravko Logarusic
Kotoko wamethibitisha kuwa wamevunja mkataba na Mcroatia, huyo, kwa makubaliano, baada ya kumpa kibarua, kilichodumu kwa miezi mitatu tu.
Siku za hivi karibuni, Loga alizuiliwa na mashabiki wa timu hiyo, kuendesha mazoezi kwa madai ya kutoridhishwa na mbinu za kocha huyo, kufuatia timu kutoka sare na Inter Allies.
Loga aliiongoza klabu hiyo ya Ghana kwa michezo 11, ambapo alishinda michezo mitano, aka droo minne na kupoteza miwili.