Kurt Zouma anastahili lawama goli la Arsenal?

Alhamisi , 13th Mei , 2021

Timu ya Chelsea usiku wa jana ilipoteza mchezo wa ligi kuu, ilipokubali kichapo cha bao 1-0 toka kwa Arsenal katika dabi ya London katika uwanja wa Stamford Bridge.

kurt Zouma

Makosa ya mlinzi Kurt Zouma katika dakika ya 16 ya mchezo yalisababisha Arsenal kupata goli lake kufuatia 'kigugumizi'cha kufanya maamuzi sahihi nani ampasie, kabla ya kuamua kuurudisha kwa kiungo wao Jorginho, ambaye naye alimrudishia kipa na kuokoa goli la kujifunga karibu na kuvuka mstari.

Ambapo mshambuliaji Pierre-Emerick Aubameyang aliuwahi na kumpasia kinda wa Kiingereza Emile Smith Rowe aliyefunga bao pekee lililiwapa ushindi, wadau wengi wanaona ni uzembe wa Kurt Zouma ndiyo umesababisha goli hilo na kuzua mjadala mkubwa.

Kwingineko Ulaya ligi ya Uhispania iliendelea kwa michezo kadhaa jumatano hii lakini mechi ya Atletico Madrid walijiweka katika mazingira mazuri ya kutwaa ubingwa baada ya kuwafunga Real Sociadad 2-1 na kufikisha alama 80 na kuendelea kuingoza katika msimamo wa ligi hiyo.

Huku wakifuatiwa na Barcelona mwenye alama 76 nyuma yake akifuatiwa na Real Madrid wenye alama 75 wakiwa pungufu mchezo 1, vita vingine vipo kwa Sevilla na Real Sociedad kugombea kuingia top 4 ili kushiriki ligi ya mabingwa Ulaya.

Nchini Italia ambapo bingwa wake amekwisha patikana ambaye ni Inter Milan, ligi iliendelea kwa michezo kadhaa usiku wa jumatano, na kushudia Ac Milan ikipata ushindi wa 7-0 dhidi ya Torino ,Juventus walipata ushindi 3-1 dhidi ya Sassuolo, Inter iliwafunga 3-1 Roma.