Messi na Ronaldo
Tiketi hii itampa muhusika fursa ya kuhudhuria sherehe ya ufunguzi kabla ya mchezo huo, na pia kukutana na wachezaji wote maarufu kama vile Ronaldo, Messi, Neymar Jr, Kylian Mbappé na wengine wengi wa PSG.
Pia watapata fursa ya kusalimiana nao na kupiga nao picha za kumbukumbu wakiwa vyumba vya kubadilisha nguo, pamoja na wakati wa sherehe za ufunguzi.
Mchezo huo wa kihistori wa kirafiki unatarajia kupigwa majira ya saa 2:00 Usiku wa leo Alhamis Januari 19, 2023 kwa saa za Afrika Mashariki.