Kiungo wa Leeds United, Kalvin Phillips.
Phillips ambaye ana mkataba na Leeds United hadi mwaka 2024, amewavutia vigogo hao baada kuonesha umahiri mkubwa wa kupora mipira na kuanzisha mashambulizi ya kushtukiza kwa kupiga pasi ndefu zenye usahihi kwa mawinga wake.
Uhodari huo umemfanya kocha wa sasa wa Mashetani wekundu, Ole Gunnar Solskjear kuonesha nia ya kumsajili Phillips ili kuimaraisha kiungo chake cha ukabaji na kuwezesha soka la mashambulizi ya kushtukiza ambalo ni mfuasi mkubwa.
Vyanzo nchini England vimeripoti kuwa Manchester United ipo tayari kutoa kitita cha paundi milioni 60 za England sawa na zaidi ya bilioni 180 za kitanzania na kutoa mkataba wa miaka 5 kwa mchezaji huyo mwenye miaka 25 sasa.
Leeds United imeonesha nia ya kutaka kumbakisha kiungo wake huyo kwa kutaka kumuongezea mkataba mnono licha ya kuwa wana mkataba naye hadi mwishoni mwa msimu wa mwaka 2024. Phillips amecheza michezo 7 na kutoa pasi 1 ya bao kwenye michezo ya michuano yote msimu huu.









