Jumatatu , 29th Mar , 2021

Nahodha wa timu ya Taifa ya Poland, Roberto Lewandowski ataukosa mchezo wa kufuzu fainali za kombe la Dunia dhidi ya timu ya Taifa ya Uingereza utakaochezwa siku ya Jumatano kutokana na kupata maumivu ya goti.

Mshambuliaji wa timu ay taifa ya Poland, Roberto Lewandowski.

Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 32, aliumia katika mchezo uliopita dhidi ya Andora ambao licha ya kufanyiwa mabadiliko alikuwa ameshaifungia nchi yake mabao mawili.

Lewandowski ambaye ameshaifungia Bayern Munich bao 42  katika michezo 36 ya mashindano yote msimu huu, anatarajiwa kuwa nje ya uwanja wa takribani siku kumi kuuguza jeraha hilo.

Nyota huyo atarejea nchini Ujerumani ambapo ataendelea kupata matibabu kabla ya kurejea dimbani.