Jumatano , 11th Nov , 2020

Mkurugenzi mtendaji wa zamani wa klabu ya Simba na mshauri wa masuala ya soka wa mwekezaji mkuu wa Simba, Mohamed Dewji Mo, ndugu Crescentius Magori amesema Simba inapaswa kujiandaa kwa mazingira yoyote yale ya changamoto na kuwa tayari kukabiliana nayo kama wana nia ya dhati ya kutaka kuw

Crescentius Magori(kushoto) akiwa na Mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi wa Simba, Mohamed Dewji (Kulia).

Akiongea katika kipindi cha Kipenga kinachoruka kila siku za Jumatatu hadi Ijumaa East Africa Radio, Magori amesema ingawa ratiba ya michuanio ya Klabu bingwa barani Afrika CAF imekuwa ni changamoto lakini Simba inapaswa kukabiliana nazo huku akiwataka wawe makini na wapinzani wao Plateau United ya Nigeria

"Ukiona timu za Afrika Magharibi inapata nafasi ya kuipeperusha bendera ya taifa lake katika mashindano ya kimataifa inabidi uwe macho sana kukabiliana nayo kwakuwa nchi kama Nigeria wana timu nzuri, mifumo bora ya kisoka na wachezaji wake wengi ni werevu na wenye viwango bora" amesema Magori

Aidha, Magori ameongeza kuwa Simba hadi sasa imeshacheza michezo kumi ya ligi hivyo anaamini hali itakuwa ni tofauti na mwaka jana ambapo waliingia katika michuano ya kimataifa kabla ya ligi kuanza hali iliyopelekea kufanya vibaya lakini hivi sasa benchi la ufundi litakuwa limeshajua ubora na mapungufu ya timu kuelekea mchezo huo.

Mapema jumahili taarifa kutoka CAF iliainisha ratiba ya michezo ya awali ya mtoano ambapo Simba itaanza ugenini dhidi ya Plateau United ya Nigeria tarehe 27, 28 na 29 Novemba na marudiano itakuwa ni kati ya tarehe 4, 5 na 6 Disemba mwaka huu.