Jumapili , 20th Jan , 2019

Wiki hii inaweza ikawa ni wiki ambayo unaweza kumtambua vizuri zaidi kocha wa zamani wa Chelsea na Manchester United, Jose Mourinho kwa maana ya falsafa zake na namna anavyojipima katika ulimwengu wa soka.

Jose Mourinho

Jose Mourinho hivi sasa anafanya kazi ya uchambuzi wa mechi za michuano ya bara la Asia pamoja na baadhi ya michezo ya Ligi Kuu nchini Ungereza ( EPL) katika televisheni ya Bein Sports.

Hii hapa ni sehemu ya kwanza ya maswali magumu ambayo Mourinho ameulizwa na kutoa majibu yake wikiendi hii.

Kwanini anatumia maneno yaliyojificha katika kutoa ujumbe kwenye mikutano yake na waandishi wa habari?

Mourinho: "ninapokuwa na Mkurugenzi wa Mawasiliano katika mfumo wa uongozi wangu, ninapenda kutumia muda wangu kuwasikiliza watu wenye maneno magumu kuliko mimi na ninapenda kuchanganya ujuzi wa wataalamu wa fani hiyo na ujumbe wangu ambao ninataka kuufikisha".

Ni mfumo gani ambao ulimpa mafaniko makubwa katika klabu ya Chelsea?

Mourinho: "kwanza kabisa nilipofika Chelsea kwa mara ya kwanza nilikuwa na mapenzi makubwa na mchezo, nilikuwa na mapenzi makubwa na klabu mpya, nilikuwa na mapenzi makubwa na mmiliki wa klabu pamoja na maono yake kwenye klabu. Pia nilikutana na C.E.O, Peter Kenyon ambaye alikuwa na maono ya hali ya juu na mahusiano yetu yalikuwa makubwa sana kwasababu mimi ninapenda kuwa na furaha ya hali ya juu".

Kwanini huwa anawakosoa sana makocha wenzake hadharani hadi kupelekea migogoro?

Mourinho: "mimi nafikiri kuwa makocha wenzangu ni watu sahihi kwangu na huwa naamini kuwa kuna sababu zilizopelekea wakateuliwa na ni kutokana na ubora wao na kitu ambacho nitafanya katika kipindi hiki nilichopo nje ya mpira ni kujizuia na kuwatetea".

Anachukuliaje namna mashabiki wa Real Madrid walivyokuwa wakimkosoa kwa mtindo wake wa kubaki basi pindi alipokuwa akiifundisha?

Mourinho: "Rekodi ya mpira wakati ule wala haikuwepo kwa Barcelona, na alieziongoza rekodi hizo ni mtu wa kujilinda, tulikwenda na kuzifunga timu zote ngumu za asili kama Barcelona, Sevilla, Atletico Madrid na Valencia na tukashinda ubingwa. nilipofika pale walikuwa wamesahau ladha ya ushindi, tukacheza fainali na Barcelona na kushinda ubingwa wa Copa del Rey ambao kwa miaka 25 walikuwa hawajashinda. nimefanya kazi nzuri katika kila klabu niliyopita".