Ijumaa , 12th Apr , 2019

Mshambuliaji wa klabu ya Yanga na timu ya taifa ya DR Congo, Heritier Makambo amefunguka juu ya uwezekano wa kuchezea timu ya taifa ya Tanzania endapo ataombwa kubadili uraia.

Heritier Makambo

Amezungumza hayo baada ya mchezo wa Ligi Kuu kati ya Yanga na Kagera Sugar katika uwanja wa CCM Kirumba Jijini Mwanza, ambao Yanga iliibuka na ushindi wa mabao 3-2.

Makambo amesema kuwa hafikirii kwa sasa kubadili uraia ili kuichezea Tanzania na hata kama ikimuhitaji hatoweza kwa sababu anajivunia na taifa lake.

"Kwangu ni furaha kuitwa katika timu ya wachezaji 40 ya taifa, hata kama nisipopata nafasi ya kucheza lakini kwangu ni kama ndoto na heshima kuwepo", amesema Makambo.

Pia akizungumzia juu ya moto wake wa kufunga katika dimba la CCM Kirumba, ambapo mpaka sasa amefanikiwa kufunga mabao matano, manne yakiwa ni ya ligi na bao moja la kombe la shirikisho, Makambo amesema,

"Kitu kinachochangia zaidi ni uzuri wa uwanja wa CCM Kirumba, unafanana na uwanja wa Taifa. Lakini pia kufunga kwangu kunaletwa na juhudi zinazofanywa na wachezaji wote wa Yanga, tunasaidiana sana ndiyo maana naweza kufunga", ameongeza.

Rekodi ya Makambo CCM Kirumba

 

Baada ya kufunga bao katika mchezo dhidi ya Kagera Sugar, Makambo amefikisha jumla ya mabao 15 ya Ligi Kuu, akimfukuzia mshambuliaji wa Mwadui FC, Salim Aiyee ambaye amefunga mabao 16.

Bonyeza hapa chini kutazama zaidi.